Saturday, September 13, 2008

Hapa ndipo mahala pa kujisetiri mpaka jua lionekane tena. Kitanda cha kuning'inia wataka nini tena?

Nani kasema majani ya shida huku? Eneo lote limezungukwa na nyasi ndefu mno, hivyo hakuna haja ya kuzileta nyumbani tena. Mara nyingi wadudu wanazifuata, nani ataka karaha ya kufukuza siafu kila siku?

Karibuni kwesui katika wilaya ya Kilindi, Tanga.
Sehemu ya kujisetiri kwa wanafamilia wa Kwesui na wageni wao. Inadhaniwa kuwa mtu akiwajisetiri hapo muda wa mchana huwa haonekani ndio maana wenyeji wameona uvivu kufunika kwa nyasi.

Nyasi za nini wakati sayansi ishamaliza yote? Harufu na watoto kucheza karibu ndio tatizo tu. Kwani wahenga walisema usichezee shilingi ....
Nyumba ya mkazi mmoja wa Kwesui, Kilindi tulipomtembelea hivi karibuni
Si Kaburi la mfalme hilo ila ni alama ionyeshayo kanisa tu

Alama ya kanisa pale Tunduru, wilaya maarufu kwa kuwa na Simba wa mjini. Wadau nisaidieni nini maana ya kuweka alama hii sehemu kama hii.
Posted by Picasa

1 comment:

Unknown said...

Hapa kweli nimepakubali sana. Yaani napatashida hasa nikiwa na kumbukumbu za Msemo ule usemao Tanga waja leo waondoka leo. Mmmh!! Hapo kweli waondoka leo.