Friday, February 01, 2008

Mauaji ya Kenya

Leo nimeona ni bora nikatoka kidogo na kueleleza maoni na masikitiko yangu kuhusu mauaji yanayoendelea kule Kenya.

Mwaka 1994 tulishuhudia mauaji makubwa katika karne iliyopita yaliyohusisha chuki za kikabila kule Rwanda. Nchi nyingi duniani ama zilikaa kimya au kuunga mkono kwa njia moja ama nyingine.

Ni jambo la kushangaza sana kuona nchi zikikaa kimya hali zikijua kabisa yanayoendelea. Labda serikali ikihusika kwenye uuaji wa raia wake wenyewe, sote twaona aibu kuikosoa. Tutakaa kimya kama vile hatusikii.

Mara kwa mara nimeona Marekeni ikijaribu kuingilia baadhi ya migogoro hapa duniani. Kile nilichosikia ni kulinda maslahi yake katika nchi hizo. Hili laweza kuwa kweli, ila maisha ya watu ni maslahi ya nani? Nani haswa atakiwaye kuingilia kati pale mmoja mwenye nguvu zaidi akim'ua mnyonge?

Laiti kama wote wangekuwa wananguvu za kijeshi walao za kushindana, sidhani kama kungekuwa na shida. Lol, hapana … nimekosea. Nishuhudiavyo mara kulipotokea hali ya aina hiyo, na kama serikali iliyo madarakani inaonekana kuelemewa. Mara moja majirani na marafiki watapeleka majeshi yao kuokoa serikali. Wale wenye silaha wataitwa waasi na watu wasiostahili kabisa.

Sasa maslahi ni Serikali zilizo madarakani ama nini? Lazima kuna jambo wafanyalo sirini. Mie sijui, weye ujuaye naomba unihabarishe.