Wednesday, October 26, 2005

Two women seeking wisdom went to a holy man. One considered herself a big sinner.

When they came to a holy man, she confess with tears while the other said none.

Holy man directed them to pick stones from a river, First one was to carry the heaviest she could carry, the other was to carry small stones she could carry.

Once they arrived the holy man told them to return them where they picked them.

One with big stone was able to return while the other woman was not able and she returned to the holy man with the sack of stones.

Small sins are easily forgotten but they are heavy to a person.

Monday, October 24, 2005

Maisha yanaanza, muda wote jicho kwenye Kompyuta, utafikiri tunataka kum'ondoa Bill Gates kwenye kiti cha utukufu. Ukiuliza ni lipi jipya umejifunza achilia mbali ulilowaletea wengine, hakuna hata kwa mwezi mmoja uliopita???

Lo, ni nini sasa unafanya muda wote huo?? Napoteza muda, ndilo jibu linalotoka.

Uwazacho ndicho huwa wewe, usipoteze muda tena, jaribu kuleta mambo mapya kwa wakaazi wa dunia hii.

Kazi njema katika kurithi utukufu wa Bill Gates. Posted by Picasa

Mambo ya Leo

Asubuhi naamka!

Mawazo yote kwenye fedha ambazo zinaonekana kupiga chenga na kujaa ahadi kem kem. Naanza kufuatilia Bingo, mvua yaanza na yanirejesha nyuma ila sikati tamaa. Leo nimeazimia kweli kweli mpaka kieleweke.

Karani anafika akiwa amechelewa kweli. Heri kuwa nilikuwa ndani. Kazi ipo sasa kuingia kwenye mstari, kila mtu naona ana picha ila mie sina. Hilo lanitatiza kwa muda. Mwishowe naamua kujitosa.

Kumbe mambo rahisi kabisa, baada ya muda nafika kuhudumiwa, kazi kama kawaida nafanikiwa.

Safari ya kurejea kuanza kufukuzia fedha nyingine walao zote zipo kwenye maandishi.

Jaza fomu, kisha kuipeleka kwa wahusika hilo lachukua kitambo kidogo.

Mwishowe naenda kwa karani wa fedha, looo kama kawaida hayupo ofisini, ila leo na staili mpya. Mlango kauacha wazi naye hayupo popote pale.
Hapo nashindwa na kurudi zangu nikiwa na wazimu wa kukosa fedha, na umasikini ndio unanizidia.

Alhamdulilah kabla ya kufunga virago jioni, napata kazi ndogo ya kusafirisha document. Malipo si hapa utafikiri naenda kwa taxi.

Sasa kwa siku kadhaa naweza kuishi, walao ijumaa yaweza fika.

Ama kweli Mola hamtupi mja wake, endelea kupambana mpaka mwisho.