Monday, October 24, 2005

Mambo ya Leo

Asubuhi naamka!

Mawazo yote kwenye fedha ambazo zinaonekana kupiga chenga na kujaa ahadi kem kem. Naanza kufuatilia Bingo, mvua yaanza na yanirejesha nyuma ila sikati tamaa. Leo nimeazimia kweli kweli mpaka kieleweke.

Karani anafika akiwa amechelewa kweli. Heri kuwa nilikuwa ndani. Kazi ipo sasa kuingia kwenye mstari, kila mtu naona ana picha ila mie sina. Hilo lanitatiza kwa muda. Mwishowe naamua kujitosa.

Kumbe mambo rahisi kabisa, baada ya muda nafika kuhudumiwa, kazi kama kawaida nafanikiwa.

Safari ya kurejea kuanza kufukuzia fedha nyingine walao zote zipo kwenye maandishi.

Jaza fomu, kisha kuipeleka kwa wahusika hilo lachukua kitambo kidogo.

Mwishowe naenda kwa karani wa fedha, looo kama kawaida hayupo ofisini, ila leo na staili mpya. Mlango kauacha wazi naye hayupo popote pale.
Hapo nashindwa na kurudi zangu nikiwa na wazimu wa kukosa fedha, na umasikini ndio unanizidia.

Alhamdulilah kabla ya kufunga virago jioni, napata kazi ndogo ya kusafirisha document. Malipo si hapa utafikiri naenda kwa taxi.

Sasa kwa siku kadhaa naweza kuishi, walao ijumaa yaweza fika.

Ama kweli Mola hamtupi mja wake, endelea kupambana mpaka mwisho.

No comments: