Tuesday, April 21, 2009
Hivi karibuni nilikuwa kule Bondeni kwenye bonde la ufa Rukwa nikiangaza sehemu za kupitisha daraja juu ya mto mkubwa wa Momba. Nimeishi kwenye kijiji cha Tululu.
Nilifanikiwa kupitia vijiji vya Chombe, Tululu, Kipeta na Kilyamatundu vya wilaya ya Sumbawanga. Hata hivyo nilifanikiwa kuvuka mto sehemu mbili za Tululu na Kilyamatundu na kwenda wilaya ya Mbozi kwenye vijiji vya Mkulwe na Kamsamba (walivuma kwa kuchuna ngozi za watu).
Vijiji vya Kilyamatundu na Kamsamba vinaunganishwa na daraja la waya (liite hivyo) japo vikajagio ni vya mbao. Daraja hili lilinishangaza sana kwa jinsi lilivyo refu na uundaji wake ulivyokuwa wa kitaalam. Heko kwa wabunifu wa daraja hili.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za daraja hili. Toa maoni.
Monday, December 08, 2008
Software Platform
I have been following new softwares as they were updated from Filehippo and come to love it, sometimes back I came accross free and open source applications website softpedia.com.
It was recently that I learn on OpenDesktop and freshmeat and GnomeFiles. I haven't spent enough time in these sites but they look promising and need recommending.
After looking at some of of these you may drop your comments on which you think is the best.
Saturday, September 13, 2008
Nani kasema majani ya shida huku? Eneo lote limezungukwa na nyasi ndefu mno, hivyo hakuna haja ya kuzileta nyumbani tena. Mara nyingi wadudu wanazifuata, nani ataka karaha ya kufukuza siafu kila siku?
Karibuni kwesui katika wilaya ya Kilindi, Tanga.
Nyasi za nini wakati sayansi ishamaliza yote? Harufu na watoto kucheza karibu ndio tatizo tu. Kwani wahenga walisema usichezee shilingi ....
Si Kaburi la mfalme hilo ila ni alama ionyeshayo kanisa tuAlama ya kanisa pale Tunduru, wilaya maarufu kwa kuwa na Simba wa mjini. Wadau nisaidieni nini maana ya kuweka alama hii sehemu kama hii.
Kinachovutia kwenye kanisa hili lililo porini ni kukosa altare na si rahisi kujua mbele ni wapi. Ni ama kwenye msalaba au njia ya kufika kanisa ilipo ndio huwa mbele ili wachelewaji waonekane.
Maandhari yake ni safi kabisa, yanafagiliwa na kufanyiwa usafi. Ila hali ya umasikini uliopo kitongojini hapa ni vigumu kabisa kuamini kama kuna mahekalu katika nchi hii.
Friday, February 01, 2008
Mauaji ya Kenya
Leo nimeona ni bora nikatoka kidogo na kueleleza maoni na masikitiko yangu kuhusu mauaji yanayoendelea kule Kenya.
Mwaka 1994 tulishuhudia mauaji makubwa katika karne iliyopita yaliyohusisha chuki za kikabila kule Rwanda. Nchi nyingi duniani ama zilikaa kimya au kuunga mkono kwa njia moja ama nyingine.
Ni jambo la kushangaza sana kuona nchi zikikaa kimya hali zikijua kabisa yanayoendelea. Labda serikali ikihusika kwenye uuaji wa raia wake wenyewe, sote twaona aibu kuikosoa. Tutakaa kimya kama vile hatusikii.
Mara kwa mara nimeona Marekeni ikijaribu kuingilia baadhi ya migogoro hapa duniani. Kile nilichosikia ni kulinda maslahi yake katika nchi hizo. Hili laweza kuwa kweli, ila maisha ya watu ni maslahi ya nani? Nani haswa atakiwaye kuingilia kati pale mmoja mwenye nguvu zaidi akim'ua mnyonge?
Laiti kama wote wangekuwa wananguvu za kijeshi walao za kushindana, sidhani kama kungekuwa na shida. Lol, hapana … nimekosea. Nishuhudiavyo mara kulipotokea hali ya aina hiyo, na kama serikali iliyo madarakani inaonekana kuelemewa. Mara moja majirani na marafiki watapeleka majeshi yao kuokoa serikali. Wale wenye silaha wataitwa waasi na watu wasiostahili kabisa.
Sasa maslahi ni Serikali zilizo madarakani ama nini? Lazima kuna jambo wafanyalo sirini. Mie sijui, weye ujuaye naomba unihabarishe.
Wednesday, January 30, 2008
Nimefurahishwa sana na matumizi makubwa ya pikipiki katika mji huu. Hata kama una gari utajitahidi tu kusafirisha mizigo kwa kutumia tuk-tuk.
Kule Songea naona walikuwa wanaelekea kuwa kama hawa kwani yeboyebo zao zilivoma sana.
Pengine ni umasikini unaosababisha haya yote, ila ni bora zaidi kama usafiri huu utakuwa salama, sheria za barabarani zikaheshimiwa na wao wakalindwa.





Nilipo kuwa Namtumbo na Tunduru katikati ya mwaka 2007.
Katika Ushoroba wa Selous - Niassa, kama waitavyo uchochoro (corridor) wa wanyama pori kati ya Mbuga za Selous ya Tanzania na Niassa ya Msumbiji.
Wednesday, October 26, 2005
When they came to a holy man, she confess with tears while the other said none.
Holy man directed them to pick stones from a river, First one was to carry the heaviest she could carry, the other was to carry small stones she could carry.
Once they arrived the holy man told them to return them where they picked them.
One with big stone was able to return while the other woman was not able and she returned to the holy man with the sack of stones.
Small sins are easily forgotten but they are heavy to a person.
Monday, October 24, 2005
Ukiuliza ni lipi jipya umejifunza achilia mbali ulilowaletea wengine, hakuna hata kwa mwezi mmoja uliopita???Lo, ni nini sasa unafanya muda wote huo?? Napoteza muda, ndilo jibu linalotoka.
Uwazacho ndicho huwa wewe, usipoteze muda tena, jaribu kuleta mambo mapya kwa wakaazi wa dunia hii.
Kazi njema katika kurithi utukufu wa Bill Gates.
Mambo ya Leo
Mawazo yote kwenye fedha ambazo zinaonekana kupiga chenga na kujaa ahadi kem kem. Naanza kufuatilia Bingo, mvua yaanza na yanirejesha nyuma ila sikati tamaa. Leo nimeazimia kweli kweli mpaka kieleweke.
Karani anafika akiwa amechelewa kweli. Heri kuwa nilikuwa ndani. Kazi ipo sasa kuingia kwenye mstari, kila mtu naona ana picha ila mie sina. Hilo lanitatiza kwa muda. Mwishowe naamua kujitosa.
Kumbe mambo rahisi kabisa, baada ya muda nafika kuhudumiwa, kazi kama kawaida nafanikiwa.
Safari ya kurejea kuanza kufukuzia fedha nyingine walao zote zipo kwenye maandishi.
Jaza fomu, kisha kuipeleka kwa wahusika hilo lachukua kitambo kidogo.
Mwishowe naenda kwa karani wa fedha, looo kama kawaida hayupo ofisini, ila leo na staili mpya. Mlango kauacha wazi naye hayupo popote pale.
Hapo nashindwa na kurudi zangu nikiwa na wazimu wa kukosa fedha, na umasikini ndio unanizidia.
Alhamdulilah kabla ya kufunga virago jioni, napata kazi ndogo ya kusafirisha document. Malipo si hapa utafikiri naenda kwa taxi.
Sasa kwa siku kadhaa naweza kuishi, walao ijumaa yaweza fika.
Ama kweli Mola hamtupi mja wake, endelea kupambana mpaka mwisho.


