Nikiwa mbele ya Kanisa Katoliki la Kambi ya Tisa kijijini Kwaluguru katika wilaya ya Kilindi, Tanga.
Kinachovutia kwenye kanisa hili lililo porini ni kukosa altare na si rahisi kujua mbele ni wapi. Ni ama kwenye msalaba au njia ya kufika kanisa ilipo ndio huwa mbele ili wachelewaji waonekane.
Maandhari yake ni safi kabisa, yanafagiliwa na kufanyiwa usafi. Ila hali ya umasikini uliopo kitongojini hapa ni vigumu kabisa kuamini kama kuna mahekalu katika nchi hii.
No comments:
Post a Comment